Loading...

3/26/2020

Marekani: Baraza la Seneti lapitisha mpango wa kuupiga jeki uchumi

Baraza la Seneti la Marekani limepitisha kwa kauli moja, mpango wa kuupiga jeki uchumi wa nchi hiyo, ili ustahimili madhara ya mripuko wa maradhi yanayosababishwa na virusi vya corona.

Baraza la wawakilishi pia linatarajiwa kuuidhinisha mpango huo wenye thamani ya dola trilioni mbili, baadaye wiki hii. Miongoni mwa mambo mengine, fedha hizo zitasaidia kuimarisha bima kwa watu ambao watapoteza ajira.

Hali kadhalika, zitatumiwa katika sekta ya afya, na majimbo ya nchi hiyo yaliyoathiriwa zaidi na virusi vya corona yatapata msaada wa mabilioni ya dola.

Vile vile makampuni na mashirika madogo na ya kadri yanaweza kuomba mikopo.

Inaelezwa pia kuwa kutoka katika fedha za mpango huo, walipakodi watapatiwa marejesho yao mara moja katika juhudi za kuchochea ufufuaji wa uchumi wa nchi hiyo.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger