Marekani yavunja rekodi ya China, Italia kwa maambukizi ya virusi vya corona

Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.

Kwa mujibu wa tawimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.

Lakini kukiwa na vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotoana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.

Idadi kubwa ya maambuizi imekujwa wakati ambao rais Donald Trump akitegemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu.

Naye makamu wa rais Mike Pence alisema kuwa vipimo vya corona virus vipo sasa katika majimbo yote 50 na zaidi ya watu 552,000 wamefanyiwa vipimo.

Bwana Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa hawafahamu idadi ya maambukizi yaiyopo China, "Hamfahamu takwimu ya maambukizi yaliyopo China."

Marekani imethibishwa kuwa na maambukizi mengi zaidi ya corona kuliko nchi nyingine yeyote duniani, kwa kuwa na visa zaidi ya 85,500.

Kwa mujibu wa tawimu za sasa zilizokusanywa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, Marekani imeipiku China ambayo ina maambukizi 81,782 na Italia yenye maambukizi 80,589.

Lakini kukiwa na vifo 1,300 vilivyotokana na ugonjwa wa Covid-19, na kuifanya Marekani ikiwa na idadi ndogo ya vifo vilivyotoana na ugonjwa huo ukilinganisha na China ambako watu 3,291 walifariki huku Italia wakiwa na vifo 8,215.

Idadi kubwa ya maambuizi imekujwa wakati ambao rais Donald Trump akitegemea kuwa hali itakuwa shwari muda si mrefu.

Je, rais Trump ana matumaini ya kuendelea na mazuio aliyoweka dhidi ya mataifa mengine
Bwana Trump alikuwa amekosolewa kwa taratibu alizoweka mpaka ifikapo sikukuu ya Pasaka, April 12.

Mipango yake inaonekana kupiga mwamba baada ya siku ya Alhamisi , maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 kuonekana kusambaa kwa kasi nchini mwake.

Siku ya Alhamisi alitangaza kuwa Wamarekani inabidi warejee kazini , nchi inabidi irejee katika hali yake ya kawaida mapema iwezekanavyo.

"Tunaweza kuchagua upande ambao hauna maambukizi sana na kuanza kuwajibika."

Aliongeza: "Watu wengi niliposema mrejee katika shughuli zenu, mlinieewa vibaya- naona waliachana na suala la kuwa mbali, kuosha mikono, kushikana mikono na kila kitu ambazo kilizuiwa.