Loading...

3/27/2020

Uuzwaji wa Chloroquine wapigwa marufuku Kenya

Wizara ya Afya Kenya imepiga marufuku maduka ya dawa na wakemia kuuza dawa za Chloroquine na Hydroxychloroquine kwa watu wasio na kibali cha kutumia dawa hizo kutoka kwa Daktari.

Agizo hilo linakuja baada ya watu nchini humo kuanza kununua dawa hizo kwa wingi kufuatia madai kuwa zinaweza kutibu corona baada ya visa vya Corona kuongezeka nchini humo.

Ikumbukwe wiki chache zilizopita rais wa Marekani Rais Donald Trump alidai Chloroquine inaweza kuwa tiba ya corona kauli ambayo imepelekea uhitaji mkubwa wa dawa hiyo Marekani na nchi nyingine.

Taarifa iliyotolewa kwa watumishi wote wa afya imesema matumizi mabaya ya madawa hiyo yanaweza kusababisha upofu wa maisha kwa mtumia bila ya kuwa na maelekezo kutoka kwa mtabibu.

Hata hivyo, wataalamu wa afya bado hawajaruhusu vidonge hivyo kutumika kwa ajili ya kutibu Virusi vya Covid 19.
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger