Afghanistan: Viongozi hasimu wakubaliana kugawana madaraka


Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani na mpinzani wake katika uchaguzi Abdullah Abdullah wametia saini makubaliano ya kugawana madaraka baada ya miezi mingi ya mtafaruku wa kisiasa.

Taarifa ya kukamilika kwa makubaliano hayo imetolewa na wasemaji wa viongozi hao. Kwa mujibu wa ujumbe kupitia mtandao wa Twittter, msemaji wa Rais Ghani, amesema Abdullah ataongoza baraza jipya la maridhiano la taifa na kwamba wanachama wa timu yake watajumuishwa kwenye baraza la mawaziri.

 Kwa upande wake msemaji wa Abdullah amesema hasimu huyo wa Rais Ghani, atashirikishwa katika serikali kwa asilimia 50. Abdullah alipinga matokeo ya uchaguzi mkuu na mzozo wa kisiasa ulifukuta baada ya wote kujiapisha kuwa marais.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items