Mwenekiti halmashauri Mbozi awataka watendaji wa Halmashauri kuhamisha dampo eneo la ujenzi kituo cha afya


Na Baraka Messa Mbozi.

MWENYEKITI  wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi,Elick Minga, ametoa siku 14 kwa watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi kuhamisha Dampo lililopo katika kata ya Ihanda ili kupisha ujenzi wa kituo cha Afya.

Alitoa agizo hilo jana baada ya kutembelea eneo hilo kufuatia mkanganyiko uliojitokeza baada ya wataalam wa idara za Afya na usafi wa Mazingira kutumia eneo hilo kama dampo ilhali awali eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Kata.

Hatua hiyo  inafuatia malalamiko ya wananchi wa Kata hiyo kulalamikia hatua ya watendaji kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Hanji Godigodi, kuvamia eneo hilo na kuanzisha Dampo bila kushirikishwa.

 "Kwa kuwa nyie watendaji wa Halmashauri mlikosea nawapa siku 14 mkae na viongozi wa kata hii ili mpendekeze sehemu nyingine  kwa ajili ya dampo na muangalie namna ya kutoa takataka hizo ndani ya muda huo, hili eneo limetengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya ambacho kitasaidia kutatua changamoto za akina mama wajawazito na watoto kutembea umbali mrefu" alisema Minga

Mwenyekiti aliwataka  watumishi wa Halmashauri kuwashirikisha wananchi katika masuala mbalimbali ili kuepusha migogoro dhidi y a wananchi wa maeneo husika.

Aidha aliwataka viongozi wa kata ya Ihanda wakishirikiana na diwani wa kata  hiyo wakishirikiana na wananchi kuanza mara moja maandalizi ya ujenzi wa kituo hicho cha afya ili kutatua changamoto ya wananchi kutembea umbali mrefu kufuata matibabu kutokana na vijiji sita kati ya nane vinavyo unda kata hiyo kukosa zahanati.

"Kata ya Ihanada ni miongoni mwa kata ambazo zina idadi kubwa ya watu katika Halmashauri ya Mbozi hivyo ujenzi wa kituo hiki cha afya utapunguza adhaa ya akina mama wajawazito kutembea umbali mrefu , viongozi wa kata hamasisheni wananchi kuanza kuandaa tofali ili ujenzi uendelee, serikali iweze kusapoti juhudi zenu na kumalizia kituo hicho" aliongeza Minga

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbozi Charles Ndimbwa alisema kuwa walikosea kupendekeza eneola dampo pasipo kuwashirikisha Viongozi wa Kata na wananchi wa kata hiyo ,na kudai kuwa watayafanyia kazi haraka maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri na kuhamisha dampo hilo ambalo linatumika na Halmashauri ya Mbozi.

"Tunaanza utekelezaji wa kuhamisha dampo kesho tutakaa na viongozi na wananchi kata ya Ihanda kuhakikisha tunapata eneo lingine ambalo litakuwa mbali na makazi ya wananchi , pia kata hii ni miongoni mwa kata zenye idadi kubwa ya watu lakini kuna upungufu mkubwa wa zahanati na kituo cha afya kwani mpaka sasa kuna zahanati mbili tu za Ihanda na Hanseketwa ndizo zinazotoa huduma"

Alisema kuwa wanaendelea kukamilisha baadhi ya zahanati katika vijiji vyote ili kutatua usumbufu wa matibabu ambao wakazi wa maeneo hayo wanayapata hivi sasa.



Kwa uapande wake Mwenyekit wa kijiji cha ihanda Maarifa Sikana alisema kuwa ukosefu wa kituo cha afya unapelekea baadhi ya akina mama kujifungulia njiani wakati wanakwenda kufuata huduma ya kujifungua katika hospital teule ya Mkoa ya Vwawa.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items