China kulipiza kisasi kwa vikwazo vya Marekani kuhusu Hong Kong


China imetishia kulipiza kisasi ikiwa itaadhibiwa na Marekani, kutokana na mipango yake ya kuweka sheria dhidi ya uasi kisiwani Hong Kong. China inapanga kupitisha sheria mpya ya usalama kuhusu Hong Kong dhidi ya uhaini, uasi na uchochezi, baada ya miezi kadhaa ya vuguvugu la maandamano ya wanaharakati wa demokrasia mwaka uliopita.

Wakaazi wengi wa Hong Kong, makundi ya biashara na nchi za Magharibi wanahofu kuwa sheria hiyo itakuwa mwisho wa uhuru katika mji huo wa kisiwa wenye utawala wa ndani, ambao ni sehemu ya China.

Marekani imeonya kuwa inaweza kuiondolea Hong Kong hadhi ya eneo lenye upendeleo wa kibiashara, baada ya polisi kutumia mabavu kuwatawanya waandamanaji, onyo lililoifanya wizara ya mambo ya nje ya China kusema italipiza kisasi dhidi ya vikwazo vyovyote vya Marekani.
Mpya zaidi Nzee zaidi