Netanyahu kuunyakua Ukingo wa Magharibi mwezi Julai


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema atayanyakua maeneo ya Ukingo wa Magharibi mnamo miezi ijayo, licha ya hatua hiyo kulaaniwa na washirika muhimu wa nchi hiyo.

Wapalestina wanalichukulia eneo zima la Ukingo wa Magharibi kama sehemu muhimu ya taifa lao la baadaye, na wanaungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

 Akiaminika kumaanisha utawala rafiki wa rais wa Marekani Donald Trump, Netanyahu amesema Israel haiwezi kuipoteza fursa ya kihistoria iliyopo ya kuchora upya ramani ya Mashariki ya Kati kwa kuufanya Ukingo wa Magharibi kuwa himaya ya Israel.

 Vyombo vya habari vya Israel vimemnukuu akisema anataka kutekeleza unyakuzi huo ifikapo mwezi Julai.
Mpya zaidi Nzee zaidi