Israel yamshtaki raia wake kwa mauaji ya familia ya Kipalestina


Mahakama moja ya Israel leo imemkuta na hatia mlowezi wa Kiyahudi kwa makosa matatu ya mauaji kufuatia shambulio la kuchoma moto, ambalo lilimuua mtoto mchanga wa Kipalestina na wazazi wake.

Mahakama hiyo imesema Amiram Ben-Uliel kutoka makaazi ya walowezi wa Kiyahudi ya Shilo, yaliyoko kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi pia ameshtakiwa kwa makosa mawili ya kujaribu kuua na kuchoma moto pamoja na kosa jingine moja la kushirikiana kutenda uhalifu unaotokana na chuki.

Mtuhumiwa huyo, alishambulia kwa kurusha bomu la moto katika kijiji cha Duma, Ukingo wa Magharibi na kumuua mtoto wa miezi 18 na wazazi wake wawili waliojeruhiwa na baadae kufa kutokana na majeraha.

Ahmed, ambaye wakati huo alikuwa na miaka minne alinusurika peke yake. Timu ya kumtetea mlowezi huyo wa Kiyahudi imesema imeiarifu mahakama kuu nchini humo kwamba itakata rufaa.

 Taarifa ya timu hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kiyahudi imeeleza kwamba hii ni siku ya kiza kwa dola la Israel, siku ambayo mahakama ya nchi hiyo imethubutu kumtia hatiani mtu ambae hana hatia.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items