Taiwan yapinga kutoshirikishwa katika mkutano wa WHO

Taiwan inapinga hatua ya kutengwa katika mkutano wa siku mbili unaofanyika kila mwaka wa baraza la shirika la afya duniani WHO unaoanza leo Jumatatu.

Taiwan na nchi nyingine kadhaa marafiki zake zimelitaka shirika hilo kuialika nchi hiyo ya kisiwa katika mkutano huo unaofanyika kwa njia ya kidigitali, kuzungumzia hatua zake za kudhibiti kirusi cha corona ambazo zinaonekana zimefanikiwa.

Waziri wa Afya na Ustawi wa Taiwan, Chen Shih-Chung ameuambia mkutano wa waandishi habari mjini Taipei kwamba ni hasara kwa WHO kwa sababu mbinu za Taiwan hazitoweza kusikika katika mkutano huo muhimu.

Kadhalika waziri huyo amesema barua ya kupinga kitendo cha kutoshirikishwa kwenye mkutano huo itapelekwa WHO mara moja.

Shirika hilo la afya duniani linakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka China na limekataa kuitambua Taiwan. Nchi hiyo ndogo ya kisiwa ina serikali yake tangu mwaka 1949 lakini Beijing inaiangalia kama sehemu ya nchi yake.

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items