Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkela wataujadili mpango wa pamoja wa kuunusuru Umoja wa Ulaya kutokana na janga la kirusi cha corona, leo ambapo mpango huo utawasilishwa wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi habari.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa Ufaransa imeeleza kwamba viongozi hao wawili watauweka wazi mpango huo wa nchi mbili wa kushughulikia janga la Covid-19 katika kiwango cha Umoja wa Ulaya katika nyanja ya afya, uchumi, mazingira na mageuzi ya kidijitali pamoja na uhuru wa kiviwanda.
Viongozi hao wawili watakutana kwa njia ya vidio katika kikao kitakachoanza alasiri ya leo.
Ulaya imeanza kuondoka kwenye hatua za kufunga shughuli zilizowekwa kuzuia usambaaji wa kirusi cha corona, hatua ambazo zimegharimu uchumi wa mataifa mengi na kuongeza uwezekano wa kutokea mporomoko mkubwa wa kiuchumi unaoweza kudumu kwa miezi kadhaa.
Hata hivyo nchi wanachama wa Umoja huo wa Ulaya kwa wiki sasa zimegawika kuhusu njia bora ya kushughulikia
