Kimbunga chasababisha maafa nchini Guatemala na El Salvador

Watu  17 wamekufa katika  kimbunga kilichotokea  nchini Guatemala na El Salvador.

Kimbunga kikubwa kilichofuatiwa na maroromoko ya ardhi nchini Guatemala na El Salvador kimesababisha  vifo vya watu  17 kulingana na taarifa za kwanza baada ya janga hilo.

Watu  15 wameuawa katika kimbunga hicho  nchini  El Salvador na wengine wawili wameripotiwa kufariki nchini Guatemala.

Kimbunga hicho kimepewa jina la Amanda  kimeacha athari kubwa nchini katika ukanda na kusababisha hasara.

Waziri wa mambo ya ndani wa El Salvador ,Mario Durna amesema kwamba watu 7 hawajulikani walipo  bada ya maporomoko ya ardhi yaliotokesa pia na kusababisha  hasara kubwa.

Watu zaidi ya  7000 wamepelekwa katika  maeneo yalio salama  ambayo  yameandaliwa kwa ajili ya kutoa hifadhi kwa watu waliobomokewa na majumba yao.

Mamlaka  imesema  majumba  900 ndio yaliobomoka kutokana na kimbunga hicho  kilichofuatiwa na  maboromoko ya ardhi.
Mpya zaidi Nzee zaidi