Liverpool jana imejihakikishia ubingwa wa Premier League msimu huu nchini Uingereza na kumaliza ukame wa miaka 30 ya kukosa taji la ligi hiyo mashuhuri baada ya Chelsea kupata ushindi wa bao 2-1 jana dhidi ya Manchester City kwenye dimba la Stamford Bridge.
Siku ya Jumatano Liverpool iliyo chini ya kocha Juergen Klopp iliibamiza bao 4 kwa nunge timu ya Crystal Palace na kuchukua uongozi wa ligi kwa pointi 23 na ilihitaji Manchester City iliyokuwa ya pili katika msimamo wa ligi kupoteza pointi ili itangazwe bingwa ikiwa imebakia michezo saba kabla ya kukamilika kwa Premier League.
Hapo jana mashabiki wa Liverpool walipuuza vizuizi vilivyoweka kukabiliana na janga la coorna na walikusanyika nje ya uwanja wa Anfiled kusherekea ushindi wa timu yao ndani ya miaka 30.
