Misri yashuhudia visa vipya 1677 vya corona ndani ya siku moja

Wizara ya afya ya Misri imetangaza karibu visa vipya 1,700 vya maambukizi ya virusi vya corona hii ikiwa ni idadi ya juu zaidi katika muda wa saa 24 tangu kugunduliwa kwa mara ya kwanza kwa virusi hivyo nchini humo katikati mwa mwezi Februari.

Wizara hiyo pia imeripoti vifo 62 vilivyotokana na ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi hivyo.Tawkimu hizo zilizotolewa jana, zinaifanya jumla ya Idadi ya maambukizi nchini humo kufikia takriban elfu 43 na vifo karibu 1500.

Misri ndilo taifa linaloongoza kwa idadi ya vifo kutokana na COVID-19 katika mataifa ya kiarabu na la tatu katika eneo la Mashariki ya Kati baada ya Iran na Uturuki.
Mpya zaidi Nzee zaidi