Kocha wa Borussia Dortmund Sebastian Kehl ametupilia mbali uvumi wa kwamba Jadon Sancho huenda akahamia Liverpool msimu huu. Manchester United pia imeonesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo, 20, wa Uingereza. (Mirror)
Kocha wa RB Leipzig, Julian Nagelsmann amesema hatma ya Timo Werner, 24, haipo tena kwenye timu hiyo. Hayo yanajiri wakati mshambuliaji huyo wa Ujerumani anasubiri kukamilisha usajili wake kuelekea Chelsea. (Mirror)
Kepa Arrizabalaga ana michuano 9 kuonesha umuhimu wake kwa timu ya Chelsea huku kukiwa na wachezaji kadhaa nyota wanaofikiriwa kujaza pengo la mlindalango huyo, 25. (Express)
Arsenal inaonekana kuwa tayari kuchukuwa ushindi katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Dayot Upamecano, licha ya kwamba Manchester United na Bayern Munich pia nazo zinamwinda mchezaji huyo, 21, wa RB Leipzig player. (Tuttosport - in Italian)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Jorginho na kocha wa Juventus Maurizio Sarri hawajazungumza tangu kocha huyo alipoondoka Chelsea lakini kiungo huyo wa kati, 28, amekuwa akihusishwa na kuhamia Ligi kuu ya soka nchini Italia, Seria A. (Daily Mail)
Mshambuliaji wa Celtic Odsonne Edouard ametupilia mbali uvumi wa kuhamia Arsenal huku mchezaji huyo, 22, akisema angependa kuwa sehemu ya timu itakayochukua taji la 10 katika klabu yake ya Scotland. (Daily Mail)

Juventus ina imani kwamba inaongeza mkataba wa mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 26, wakati mchezaji huyo anaomba kufikiwa kwa makubaliani ya £11m kwa mwaka. (Goal)
Kocha wa Mainz Rouven Schroder anasema klabu hiyo iko katika mazungumzo ya kuendeleza mkataba wa mshambuliaji wa Liverpool forward Taiwo Awoniyi. Raia huyo wa Nigeria, 22, amekuwa Bundesliga kwa mkopo tangu msimu uliopita.
Kiungo wa kati raia wa Chile, Arturo Vidal, 33, amesema kuwa atafurahishwa na hatua ya kuhamia Inter Milan, akisema anahisi kwamba hana umuhimu katika timu ya Barcelona. (Goal)
Mshambuliaji Edinson Cavani, 33, ataondoka Paris St-Germain pamoja na mlinzi Thiago Silva, 35, mwisho wa Agosti, mkurugenzi wa klabu hiyo amethibitisha. (Le Journal du Dimanche - in French and subscription only)