Uturuki yatoa msaada wa vifaa vya matibabu nchini Iraq kama ishara ya ushirikiano
Uturuki imetuma vifaa vya matibabu na madawa nchini Irak kuonesha ushirikiano katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.
Balozi wa Uturuki mjini Baghdad nchiniIrak Fatih Yılmaz amesema kuwa msaada huo umetolewa nchini humo kwa lengo la kupunguza athari za maambukizi na kuzuia maambukizi kuendelea katika jamii.
Msaada huo wa madawa na vifaa vya matibabu ni kwa ajili ya hospitali za zahanati ambazo zimekumbwa na uhaba wa madawa.
Balozi huyo wa Uturuki nchini humo Iraq amenndelea akisema kwamba katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na maambukizi ya virusi vya corona , Uturuki imejitolewa kadri na uwezo waek kuwa karibu na mataifa ambayo yalihitaji msaada katika kupambana na covid-19.
Wakti ambapo visa vipya vikiendelea kuripotiwa nchini humo , idara ya afya imekumbwa na changamoto kubwa kutokana na uhaba wa vifaa vya matibabu.
Kutokana na uhaba huo, waziri mazingira na jamii ameomba msaada kutoka Uturuki ilikuweza kumudu ombi kubwa la madawa katika hospitali tofauti.
Rais ErdoÄŸan amesema kwamba ni jukumu kwa Uturuki kuonesha ushirikiano na majirani zake katika kukabiliana na janga la corona.
Ni watu 839 nchini Irak ambao wamekwishafariki kutokana na maambukizi ya virusi vya corona huku watu walioambukiwa idadi yake ikitajwa kuwa watu 47 151.