James Kaji athibitishwa kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amemthibitisha Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, James Kaji, kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, leo Julai 06, 2020.