Jumuiya ya Polisi Waislamu Uingereza yapendekeza kufutwa neno "Kiislamu" wakati wa kutaja ugaidi


Jumuiya ya Kitaifa ya Polisi Waislamu nchini Uingereza imependekeza kufutwa sifa ya "Kiislamu" wakati linapotokea shambulizi la kigaidi ili kuzuia propaganda chafu dhidi ya dini hiyo.
Jumuiya hiyo imetangaza kuwa, kuyasifu mashambulizi ya kigaidi au magaidi kuwa ni "ugaidi au magaidi wa Kiislamu" au "kijihadi" ni ubaguzi na kudhalilisha dini tukufu ya Uislamu.
Afisa wa Jumuiya ya Kitaifa ya Polisi Waislamu ya Uingereza Alexander Ghent Alexander Ghent amesema kuwa, polisi ya Uingereza inapaswa kubadili utamaduuni na utaratibu wa kuripoti mashambulizi ya kigaidi na kujiepusha kufungamanisha ugaidi ya dini ya Uislamu na jihadi. 
Takwimu zinaonyesha kuwa, uhalifu na jinai zinazotokana na chuki dhidi ya Waislamu zimeongezeka sana katika jamii za watu wa Ulaya katika miaka ya hivi karibuni na baadhi ya jumuiya na makundi ya Kiislamu nchini Uingereza yanaamini kuwa, serikali ya nchi hiyo haina azma thabiti ya kukabiliana na chuki na propaganda chafu dhidi ya Uislamu.

Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Kiislamu ya Haki za Binadamu nchini Uingereza (IHRC) yenye makao yake makuu London anasema kuwa propaganda chafu dhidi ya Uislamu zimevuka suala ya kuchafua sura ya dini hiyo na kufikia kiwango cha kueneza chuki na uhasama dhidi ya Waislamu. 
Massoud Shajareh ameongeza kuwa, uzembe na kimya cha wanasiasa mbele ya mashambulizi yanayowalenga Waislamu na kupuuza sheria za kukabiliana na ugaidii vimezidisha mashambulizi dhidi ya Waislamu nchini humo.
Mpya zaidi Nzee zaidi