https://monetag.com/?ref_id=TTIb Mahakama ya Afrika yaamuru Tanzania kuruhusu kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi | Muungwana BLOG

Mahakama ya Afrika yaamuru Tanzania kuruhusu kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi

Mahakama ya Afrika inayohusiaka na masuala ya haki za imeiamuru Tanzania kukifanyia mabadiliko kipengele cha katiba yake ambacho kinaizuia mahakama yoyote kuchunguza uchaguzi wa rais baada ya mshindi kutangazwa rasmi.

Wakili wa Tanzania, Jebra Kambole aliwasilisha kesi katika mahakama hiyo ya Arusha mwaka wa 2018 akihoji kuwa kipengele hicho kinakiuka haki zake.

Katiba ya Tanzania inaeleza kuwa mara baada ya mgombea wa urais atatangazwa mshindi na tume ya uchaguzi, "hakuna mahakama yoyote ya kisheria itakuwa na mamlaka ya kuchunguza uchaguzi wa mgombea huo." Mahakama nchini Kenya na Malawi ziliyabatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais uliowapa ushindi viongozi waliokuwa madarakani, kutokana na makosa, na kulazimisha kurudiwa kwa uchaguzi, katika kile kinachoonekana kuwa ushindi kwa demokrasia barani humo.

Taarifa ya mahakama hiyo pia imeiamuru Tanzania kuwasilisha ripoti katika miezi 12 kuhusu hatua ilizochukua za kutekeleza uamuzi huo na kuamuru kuwa nchi hiyo lazima ichapishe uamuzi huo kwenye tovuti ya wizara ya masuala ya sheria na katiba katika kipindi cha miezi mitatu.