Rais wa Urusi Vladmir Putin, amewashukuru Warusi baada ya kuidhinisha kwa kishindo marekebisho ya katiba ambayo yatamruhusu kurefusha utawala wake hadi 2036.
Putin amelihutubia taifa kupitia televisheni baada ya tangazo kutoka tume ya uchaguzi ya Urusi kuwa karibu asilimia 78 ya wapiga kura waliunga mkono marekebisho ya katiba.
Rais huyo amesisitiza kuwa mabadiliko hayo yalihitajika kwa sababu yanaimarisha mfumo wa kisiasa na kuboresha huduma za kijamii pamoja na kuongeza nguvu uhuru wa nchi hiyo.
Hakutaja chochote kuhusu ukweli kwamba mabadiliko hayo pia yatauweka upya ukomo wa muhula wake kikatiba, yakimruhusu kubakia madarakani kwa miaka mingine 12 baada ya kumalizika kwa muhula wake wa sasa mwaka wa 2024.