Rais wa Mali kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa


Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita ametangaza kuanzisha mchakato wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa katika nchi hiyo inayoandamwa na machafuko baada ya kupata shinikizo kutoka viongozi wa mataifa ya Afrika Magharibi.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Mali imesema ili kukidhi matakwa ya jumuiya ya kikanda ya ECOWAS, rais Keita ameamua kuunda ujumbe wa mawaziri wachache watakaopewa jukumu la kufanya majadiliano na upande wa upinzani kwa lengo kuunda serikali ya pamoja.

 Waandamanaji wamekuwa mitaani kwa wiki kadhaa sasa kushinikiza kujiuzulu kwa rais Keita ambaye uongozi wake unaandamwa na kitisho cha makundi ya itakadi kali na uchumi unaodorora.

 Hapo kabla viongozi wakuu wa nchi 15 za jumuiya ya maendeleo ya nchi za magharibi ya Afrika, ECOWAS, walisema wanamuunga mkono rais Keita lakini wakatoa wito wa kuundwa serikali ya pamoja itakayojumuisha upande wa upinzani.
Mpya zaidi Nzee zaidi