Rouhani aelezea matumaini ya kutekelezwa mkataba wa nyuklia wa 2015

Rais wa Iran, Hassan Rouhani ameelezea matumaini yake kuwa ushirikiano wa kimataifa huenda ukasababisha utekelezwaji mzuri wa mkataba wa nyuklia uliosainiwa mwaka wa 2015.

Rouhani amesema makubaliano ya nyuklia yanaashiria thamani ya mikataba ya kimataifa wakati akiadhimisha miaka mitano ya kusainiwa mkataba huo.

Amesema ni matumaini yao kwamba maadili ya aina hiyo ya kimataifa hayataharibiwa na sera za Marekani na kuwa nchi zilizotia saini zitaweza kuutekeleza.

Amelaumu udhaifu wa sasa kwenye mkataba huo kusababishwa na kile amekiita kundi hatari la pande tatu, Saudi Arabia, Marekani na Israel ili kuichochea Iran kujiondoa ili wailaumu Tehran kwa kuvunjika kwake.

Mkataba huo wa nyuklia ulinuia kuiwezesha Iran kuwa na mpango wa nyuklia wa matumizi ya kiraia, wakati ukizuia silaha za nyuklia, katika kubadilishana na kuondolewa vikwazo vinavyouathiri uchumi
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items