Leo tarehe 15/07/2020 Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza amechukua na kurejesha fomu ya kuwania ubunge wa Viti Maalumu mkoa wa Songwe ambapo Mhe. Shonza anaingia kwenye kinyang'anyiro hicho kutetea nafasi yake ya kuendelea kuwawakilisha wakinamama wa Mkoa wa Songwe aliyoitumikia kwa miaka mitano tangu 2015 hadi 2020.
Mhe. Shonza amechukua fomu hiyo katika ofisi za UWT mkoa wa Songwe ambapo amekabidhiwa fomu na Katibu wa UWT mkoa Bi. Camila Kigosi.
Mhe. Shonza amechukua fomu hiyo katika ofisi za UWT mkoa wa Songwe ambapo amekabidhiwa fomu na Katibu wa UWT mkoa Bi. Camila Kigosi.