Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani amesema kuwa, siasa za Rais Donald Trump wa nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiyo sababu ya kushindwa Washington katika medani zote.
Leon Panetta amesema kuwa siasa za Donald Trump za kutaka kupindua mfumo wa utawala nchini Iran hazijafua dafu, na Washington imeshindwa katika medani zote.
Awali Panetta alikosoa misimamo ya rais wa sasa wa Marekani na kusema kuwa, Donald Trump ameacha kukabiliana na changamoto na migogoro migumu ya kipindi cha sasa na kuelekeza nguvu zake kwenye uchaguzi ujao wa rais.
Awali Panetta alikosoa misimamo ya rais wa sasa wa Marekani na kusema kuwa, Donald Trump ameacha kukabiliana na changamoto na migogoro migumu ya kipindi cha sasa na kuelekeza nguvu zake kwenye uchaguzi ujao wa rais.
Tarehe 8 Mei mwaka 2018 Rais Donald Trump wa Marekani aliiondoa nchi hiyo katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA na akatoa amri ya kurejeshwa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Baada ya hapo Trump aliahidi kuiburuta Iran kwenye meza ya mazungumzo kwa ajili ya mapatano mapya kwa kutumia siasa za "mashinikizo ya kiwango cha juu". Hata hivyo kiongozi huyo amefeli vibaya katika siasa hizo na amekuwa akikosolewa sana na makundi mbalimbali ndani na nje ya Marekani hususan katika kipindi hiki cha kabla ya uchaguzi wa rais wa Novemba mwaka huu.
Wakosoaji wa Trump wanamlaumu kwa kutokuwa na stratejia mkabala wa Iran, kuzidisha mivutano isiyo na maana na kuitenga Marekani na washirika wake muhimu.

