Mamlaka nchini Ujerumani zinampango wa kuweka vipimo vya virusi vya corona katika viwanja vyake vya ndege kwa ajili ya wasafiri ambao wanatoka katika mataifa yenye kitisho zaidi cha maambukizi hayo.
Uamuzi huo umefikiwa na maziri wa afya wa majimbo 16 ya Ujerumani unatokana na uwepo wa wasiwasi kwamba watu wanaorejea kutoka katika matembezi ya likizo ya msimu huu wa kiangazi watarejesha virusi hivyo kutoka katika maeno watokako.
Lakini pia kuna wasiwasi kwamba sio kila mtu, anaetoka katika maeneo yalioainishwa kuwa ya hatari anaweza kujitenga pasipo kufanyiwa vipimo.
