Loading...

Jul 4, 2020

Vituo 74 vilivyotengwa kwaajili ya wagonjwa wa corona vyafungwa

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu  amefunga kituo cha Lulanzi Mkoani Pwani kilichokuwa kimetengwa kwa ajili ya wagonjwa wa Corona baada kutokuwa na mgonjwa toka May 26, 2020, sasa Hospitali hiyo inarudisha huduma za afya za kawaida kwa Wananchi wa Kibaha na maeneo jirani.

Kituo cha Lulanzi,Pwani kilikua ni moja ya vituo vikubwa vilivyotengwa kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa Corona kikitanguliwa na vituo vya Amana, Mloganzila na Temeke, pia kimekua kituo cha 74 kufungwa kati ya 85 ambavyo vilitengwa Nchi nzima na sasa Tanzania imebakiwa na vituo 11 vya Corona.

“Zimebaki kambi 11 tu zikiwemo Hospitali binafsi, hili ni jambo la kumshukuru Mungu, ombi langu ni kwamba tusibweteke, tuendelee kujikinga ili Watu wasipate maambukizi” -WAZIRI UMMY
KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger