Na Faruku Ngonyani ,Mtwara
Wananchi wa Mkoa wa Lindi wapokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamini William Mkapa kilichotekea usiku wa Tarehe 24 julai 2020.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi alipowasili Kijiji cha Lupaso Wilayani Masasi eneo ambalo mazishi ya hayati Mkapa yatakapofanyikia.
Zambi amesema kuwa Benjamini Mkapa ni kiongozi ambaye atakayekumbukwa kwa mambo mengi aliyoyafanya enzi za uongozi na uhai wake kwa hapa nchini Tanzania na nje ya nchi pia.
Lakini pia Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Benjamini Mkapa atakumbukwa kwa kuifanya Tanzania kuwa na mabadiliko ya kiuchumi kwa kuanzisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambapo kwa kiasi kikubwa Taasisi hizo zimesaidia kuongeza makusanyo ya kodi hapa nchini.
Ikumbukwe hayati Benjamini Mkapa alikuwa mkulima wa zao la korosho katika Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi hivyo Mkoa huo umepata pigo la kuondokewa na mzalishaji wa kiuchumi kupitia zao hilo
