Maafisa nchini Belarus wamefuta vibali vya wanahabari wa vyombo kadhaa vya kigeni, kabla ya maandamano ya hivi karibuni kabisa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.
Msemaji wa serikali Anatoly Glaz amesema uamuzi huo umechukuliwa kufuatia mapendekezo ya kitengo cha nchi hiyo cha kupambana na ugaidi. Hakufafanua ni wanahabari wangapi walioathirika na hatua hiyo, lakini vyombo vya kigeni vikiwemo BBC na Radio Liberty viliripoti kuondolewa kwa vibali vya wanahabari wao kadhaa. \
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka wa 1994, anakabiliwa na vuguvugu lisilo la kawaida la maandamano tangu uchaguzi unaopingwa wa Agosti 9 ambao alipata ushindi wa kishindo wa asilimia 80 ya kura.
Upinzani umeandaa mtukio mawili ya maandamano makubwa mwezi huu na umeitisha maandamano ya kiwango kikubwa kesho Jumapili.