DC Seleman Mzee atoa wito kwa wizara ya mifugo na uvuvi

Na Ahmad Mmow, Ngongo. 

 Katika kuhakikisha wasomi wanajiajiri kupitia uvuvi na ufugaji. Wizara yenye dhamana ya mifugo na uvuvi imeshauriwa iwatambue na kuwasaidia wasomi hao ambao wameamua kujiajiri kupitia sekta hizo. 

Ushauri huo umetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Masasi, mkoa wa Mtwara Seleman Mzee Seleman alipotembelea mabanda ya maonesho ya wakulima(NANENANE) kanda ya Kusini. Ambapo alitoa ushauri huo baada ya kufika katika banda la wizara ya mifugo na uvuvi ambalo lipo eneo la Ngongo, manispaa ya Lindi. 

 Seleman alisema sekta za mifugo na uvuvi inaweza kuchangia kwakiasi kikubwa  kupunguza changamoto ya ajira kwa baadhi ya wasomi ambao wameamua kujiajiri. 

Kwahiyo wizara iwatambue na kuwasaidia ili wafikie malengo yao. 

Mbali na ushauri huo, mkuu huyo wa wilaya ya Masasi alitoa wito kwa wizara kuwakuza wajasiriamali, hasa waliokwenye vikundi vya ujasiriamali. 

Huku akishauri ishirikiane na halmashauri kuwatafutia masoko ya ndani nanje ili wajiingizie vipato vyao na taifa. 

Seleman hakuishia hapo, bali alishauri wataalamu wanaokuwepo kwenye maonesho wasiishie kwenye maonesho pekee. 

Bali walau mara chache waende katika halmashauri wakaone matokeo ya elimu wanayotoa kwenye maonesho hayo.

Kwani halmashauri nyingi zina changamoto ya uhaba wa maofisa ugani. Kwani kuna umuhimu wa kufanya tathimini ili kuona matokeo ya maonesho ya kila mwaka. 

 Maonesho ya Nanenane kanda ya Kusini yanayoshirikisha mikoa ya Lindi na Mtwara yanafanyika katika viwanja vya Ngongo, manispaa ya Lindi kila mwaka.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi