Loading...

Aug 1, 2020

Hatma ya Mbao, Mbeya City, Ihefu na Geita ni leo


Vilabu vya Mbao Fc ya Mwanza, Mbeya City ya Mbeya zote za ligi kuu pamoja na Ihefu ya Mbeya pia Geita Gold ya Geita vitafahamu hatma yao juu ya nafasi ya kucheza ligi kuu msimu ujao baada ya michezo yao itakayopigwa jioni.


Mbao ambayo ilikua haijapoteza katika mechi tisa za mwisho za VPL, ilikumbana na kipigo cha mchezo wa mtoano dhidi ya Ihefu cha bao 2-0, hivyo ili inusurike kushuka daraja itabidi ipate ushindi wa bao 3-0 katika mechi ya marudiano itakayochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Kwa upande wa Geita Gold, yenyewe itahitaji ushindi na si vinginevyo kama itahitaji kupanda ligi kuu, vile vile Mbeya City itakua inahitaji matokeo chanya baada ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa mondo wa kwanza uliopigwa mkoani Geita.

Mbao na Mbeya City ziliangukia katika michezo ya mtoano baada ya kumaliza kwenye nafasi za 15 na 16 kwenye msimambo wa VPL huku Geita na Ihebu zilimaliza washindi wa pili kwenye makundi ya Ligi daraja la kwanza msimu uliomalizika.

KWA HABARI, LIVE TV, RADIO, MATOKEO YA LIGI ZOTE DUNIANI DOWNLOAD APP YA MUUNGWANA BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger