Mahakama ya Umoja wa Mataifa kutoa hukumu katika kesi ya kuuwawa Hariri


Mahakama inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa nchini Uholanzi inatoa hukumu leo katika kesi inayowahusu watu wanne ambao hawapo mahakamani; 


wanachama wa kundi la wanamgambo wa Hezbollah ambao wanatuhumiwa kuhusika katika shambulio la bomu lililomuuwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.Hukumu hiyo ilicheleweshwa kwa karibu wiki mbili ikiwa ni kutoa heshima kwa wahanga wa mripuko mwingine, katika bandari ya mjini Beirut.

 Mripuko wa hapo Agosti 4 umesababisha vifo vya watu 180, na kuwajeruhi wengine zaidi ya 6,000, na zaidi ya watu robo milioni nyumba zao hazifai tena watu kuishi, katika taifa hilo ambalo tayari lilikuwa likitaabika kutokana na hali mbaya ya kiuchumi na kijamii. 

Hukumu itakayowapata watuhumiwa kuwa na hatia inaweza kuzidisha hali ya wasi wasi nchini humo.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi