Ndege za Israel zashambulia Gaza


Jeshi la Israel limesema ndege zake za kivita zimeshambulia eneo la Gaza linaloongozwa na Hamas mapema leo kujibu mashambulizi ya maputo ya moto kutoka kwa Wapalestina katika mpaka. 

Duru za Hamas zimesema mashambulizi yanakuja wakati maafisa wa usalama wa Misri wakifanya ziara katika eneo hilo kujaribu kupunguza hali ya kuongezeka kwa ghasia. 

Taarifa ya jeshi la Israel imesema ndege za kivita na ndege nyingine zimeshambulia miundo mbinu ya chini ya ardhi inayomilikiwa na kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza. 

Duru za Hamas zimeliambia shirika la habari la AFP kwamba kundi hilo limefanya mazungumzo na ujumbe wa Misri mjini Gaza jana kabla ya ujumbe huo kuondoka katika eneo hilo kwenda kufanya mkutano na Waisrael na mamlaka ya Palestina katika ukingo wa magharibi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi