Mamlaka ya taifa ya hali ya hewa nchini Marekani NWS, imerekodi kiwango cha juu cha joto katika eneo la Death Valley mjini California kilichofikia nyuzi joto 54.4 katika kipimo cha Selshasi.
Katika taarifa yake mamlaka hiyo imesema vipimo hivyo ni vya awali na endapo vitathibitishwa, basi itakuwa ndio kiwango cha juu cha joto kuwahi kushuhudiwa katika eneo la Death Valley tangu Julai 1913.
Mamlaka ya hali ya hewa duniani WMO, ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya hali ya hewa, tabia nchi na maji, imesema kuwa itathibitisha kiwango hicho cha joto ambacho huenda kikavunja rekodi ya dunia tangu mwaka 1931.
Joto la juu kabisa lililowahi kurekodiwa eneo la Death valley lilikuwa ni nyuzi joto 134 kipimo cha Fahrenheit, ambacho mpaka sasa ndio kiwango cha juu duniani kulingana na WMO.
