Michelle Obama amemshambulia kwa maneno Rais wa Marekani Donald Trump wakati chama cha Democrats kimeanza rasmi kampeni yake ambapo Joe Biden ndiye aliyetwikwa jukumu la kuwa mgombea wa chama hicho kuelekea Ikulu.
"Donald Trump sio rais sahihi kwa nchi yetu," amesema aliyekuwa mama taifa wa Marekani katika ujumbe wake wenye hisia uliorekodiwa wakati wa mkutano chama cha Democratic.
Waasi wa chama cha Trump cha Republican pia nao hawakusita kutoa yaliyo moyoni wakati wa mkutano huo.
Bwana Trump ambaye yuko nyuma ya Biden katika kura ya maoni, Michelle amesema.
Kwasababu ya mlipuko wa virusi vya corona, Democrats ilifutilia mbali mkutano uliokuwa umepangwa kufanyika na shughuli zingine zote za kisiasa huko, Milwaukee, Wisconsin.
Lakini bado hijafahamika ikiwa mikutano hiyo kwa njia ya mtandao ambayo hotuba zake zimerekodiwa na bila uwepo wa watu wanaoshuhudia moja kwa moja kunaweza kusababisha msisimko ule ule kama ya wakati wa kabla ya janga la corona.
Chama cha Republican kitakumbana na changamoto hiyo hiyo wakati wanathibitishia umma umuhimu wao wa kuwa uongozini katika kipindi cha miaka minne kwenye mkutano wao uliopangwa kufanyika wiki ijayo.
