Netanyahu ashutumu vyombo vya habari kuhusu maandamano dhidi yake

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaumu maandamano yanayozidi kuongezeka dhidi ya utawala wake, akisema yanachochewa na vyombo vya habari vyenye kuegemea upande mmoja vinavyopotosha ukweli na kuwahimiza waandamanaji.

Netanyahu amekabiliwa na wimbi la maandamano katika wiki za karibuni, ambapo waandamanaji wanashinikiza kiongozi huyo wa muda mrefu, na alieshtakiwa kujiuzulu, hali hiyo ikichochewa pia na namna serikali yake ilivyoshughulikia janga la virusi vya corona.

Netanyahu hata hivyo, ameyataja maandamano hayo kuwa viota vya wafanya fujo na wafuasi wa mrengo wa kushoto wanaopania kumpindua kiongozi huyo wa siasa za mrengo wa kulia. Akiongea kwa ghadhabu wakati wa mkutano wa baraza lake la mawaziri, Netanyahu amevikosoa vyombo vya habari kwa kuchochea maandamano hayo na kwa kupotosha ukweli wa matukio ya vurugu dhidi ya waandamanaji.