Dodoma "Nitafanya kazi na kuendeleza pale alipoishia Rais Ally Mohamed Shein. Nitakwenda kwa 'speed'" - Mgombea urais CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ally Mwinyi.
"Wanachama wa CCM nawaomba tusibweteke kwa kuwa tunakwenda kushinda kwenye uchaguzi mkuu, kikubwa tujitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura" Mgombea urais CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ally Mwinyi.
"Niwaombe Watanzania tuhakikishe tunailinda amani, bila amani hakuna maendeleo, Kuna baadhi ya wanasiasa wameanza kutoa kauli za uvunjifu wa amani, Niwaombe tuwapuuze kwani amani ya nchi inajengwa na wananchi wake". Mgombea urais CCM Zanzibar, Dk. Hussein Ally Mwinyi.
