Rais wa Uturuki ampokea mkuu wa baraza kuu la Libya



Halid al Mashri, mkuu wa baraza  kuu la Libya katika ziara yake nchini Uturuki amepokelewa na rais Recep Tayyıp ErdoÄŸan  mjini Istanbul.

Halid al Mashri  amewasili Uturuki Alkhamis ambapo amefanya mazungumzo na rais ErdoÄŸan na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Uturuki.

Katika mazungumzo yao , viongozi hao wa wamejadili kuhusu masuala tofauti kuhusu ushirikiano kati ya Uturuki na Libya.

Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt ÇavuÅŸoÄŸlu amezungumza pia na  Halid al Mashri.

Katika ujumbe wake aliotoa katika ukurasa wake wa Twitter, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kwamba  ushirikiano kati ya Uturuki na Libya unazidi kuimarika siku hadi siku.

Katika mazungumzo yao viongozi  hao wamezungumzia pia kuhusu ushirikiano katika sekta ya uchumi na biashara na ulinzi.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi