Wachezaji wa mpira wa vikapu Marekani wasusia michuano ya fainali

Wachezaji wa kulipwa wa mchezo wa mpira wa vikapu wanaume na wanawake hapa Marekani wamesusia wiki hii kushiriki kwenye michuano ya finali ambayo imekuwa ikiendelea wakilalamika dhidi ya polisi kumpiga risasi Jacob Blake Mmarekani Mweusi katika mji wa Kenosha, jimbo la Wisconsin mwishoni mwa wiki.

Shirikisho la kitaifa la mpira wa vikapu la wanawake WNBA liliahirisha mechi 3 Jumatano baada ya timu ya Washington Mystics kususia mechi yao dhidi ya timu ya Atlanta Dreams wakilalamikia dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Msimamo huo ulifuatia uamuzi wa awali wa shirikiso la wanaume NBA kusitisha michuano baada ya baadhi ya timu kususia mechi zao dhidi ya tukio hilo hilo.

Baada ya kufanya uamuzi wa kutoshiriki kwenye mechi hizo, wachezaji kutoka timu ya washington ya Mystics pamoja na wenzao wa WNBA, walijitosa kwenye viwanja, ili kuonyesha wazi malalamiko yao huku baadhi wakipiga goti huku wengine wakivalia t-shirt zenye maandishi ya Black Lives Matter.
Mpya zaidi Nzee zaidi