Merkel angependelea hatua kali kuzuia kuenea COVID-19


 Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema angependelea kukubaliana kuhusu hatua kali za kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona na viongozi wa serikali ya shirikisho na za majimbo. 

Akizungumza leo baada ya mkutano wake na viongozi hao uliofanyika jana, Merkel amesema ana wasiwasi kuhusu kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona kwenye maeneo kadhaa ukiwemo mji mkuu, Berlin. 

Kansela huyo wa Ujerumani amesema kila siku ni muhimu katika kupambana na virusi vya corona. Katika mkutano wa jana, viongozi wa shirikisho na majimbo walikubaliana kuahirisha kuchukua hatua kali za kukabiliana na janga la COVID-19 hadi katika mkutano wao uliopangwa kufanyika Novemba 25. 

Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ya Ujerumani, Robert Koch imethibitisha kuwa visa vya virusi vya corona vimeongezeka hadi 14,419 katika kipindi cha saa 24, huku vifo vikiongezeka na kufikia 267.


Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items