Waziri Mkuu wa Ethiopia kuanzisha mashambulizi ya mwisho Tigray

 


Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed amesema operesheni ya mwisho na muhimu ya kijeshi itaanzishwa katika siku zijazo dhidi ya serikali ya waasi wa jimbo la Tigray. 

Abiy amesema siku tatu za mwisho zilizowekwa kwa viongozi wa Tigray na vikosi maalum vya jimbo hilo la kaskazini, zinamalizika leo. 

Waziri mkuu huyo wa Ethiopia ameendelea kupuuza wito wa kimataifa wa kufanyika mazungumzo na kuzuia mashambulizi hayo ya wiki mbili ambayo yameingia katika nchi jirani za Eritrea na kusababisha zaidi ya Waethiopia 25,000 kukimbilia Sudan, kusambaa zaidi. 

Nchi jirani za Uganda na Kenya zimetoa wito wa kupatikana suluhisho la amani, lakini serikali ya Abiy inaichukulia serikali ya Tigray kama isiyo halali, baada ya kukaidi na kufanya uchaguzi mwezi Septemba uliokuwa umeahirishwa kwenye maeneo mengine ya nchi.


Post a Comment

0 Comments