Mwanamfalme, maarufu wa Saudi Arabia, Turki al-Faisal, leo hii ameikosoa vikali Israel, katika mkutano wa kilele wa usalama wa Bahrain, ambao pia umehudhuriwa na waziri wa mambo ya nje wa Israel.
Mwanamfalme Al-Faisal, ambae aliwahi kuongoza kitengo cha intelijensia cha taifa lake kwa zaidi ya miongo miwili na pia kuhudumu kama balozi wa Marekani na Uingereza amesema aina yoyote ya makubaliano ya kurejesha mahusiano ya kidiplomasia yanahitajika kuisaidia Palestina kupata uhuru wake.
Amelifananisha taifa la Israel kama "Ukoloni wa Magharibi" akisema Israel imewafunga Wapalestina wake kwa waume katika kambi ya mateso pasipo kufutwa kwa mkondo wa sheria.
Wanavunja makazi ya wapalestina kwa kadri watakavyo na pamoja na kuwauwa. Ingawa Mwanamfalme huyo hana cheo chochote kwa sasa lakini msimamo wake unaonekana kuakisi fikra za Mfalme Salman wa Saudi Arabia.
Saudi Arabia imekuwa ikisisitiza hatua yoyote ya kufanikisha mahusiano ya kidiplomasia kati yake na Israel, itafanyika endapo kutakuwepo na makubaliano ya muda mrefu ya amani yatakayohusisha kile ilichokiita "suluhisho la mataifa mawili" katika mgogoro wa Palestina na Israel.
