China yaitaka India kumrejesha askari wake inayemshikilia

 


China imetaka kuachiliwa kwa askari wake anayedaiwa kushikiliwa na mamlaka za India baada ya kupotea katika maeneo ya mpaka. Baada ya China kuripoti juu ya kupotea kwa askari wake, India ilikiri kumshikilia askari huyo na kuongeza kuwa ingemrejesha mara baada ya kupokea maagizo kutoka ngazi ya juu. 


Taarifa kutoka kwa Jeshi la India inadokeza kuwa askari wa China alikamatwa Ijumaa kwa kukiuka sheria na kuingia upande wa India katika eneo la Kusini mwa Ziwa Pangong Tso. 


Mvutano uliibuka kati ya China na India mnamo Juni mwaka jana wakati makabiliano ya mpakani kwenye jimbo linalozozaniwa la Himalaya kusababisha vifo vya askari 20 wa India. Miezi iliyofuata mataifa hayo jirani yaliyojihami kwa silaha za nyuklia yalipeleka maelfu ya askari wake katika mipaka yake.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi