Raia wa Qatar wameanza kuingia Saudi Arabia leo Jumamosi kupitia mipaka iliyofunguliwa siku chache baada ya muungano wa nchi unaongozwa na Saudia kuhitimisha vizuizi dhidi ya Doha.
Viongozi wa nchi tatu za Ghuba za Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain pamoja na Misri walitia saini makubaliano na Qatar katika mkutano wa kila mwaka wa nchi za Ghuba, kumaliza mgogoro uliodumu miaka mitatu na nusu.
Saudi Arabia ilikubali kufungua mpaka wake na Qatar na pia kuruhusu safari za ndege ikiwa ni hatua kubwa katika mzozo wa mataifa ya Ghuba.
Mwaka 2017, mataifa hayo yalivunja uhusiano wa kidiplomasia, biashara na usafiri na Qatar baada ya kuishutumu kuwa inauunga mkono vikundi vya wapiganaji wa Kiislamu, shutuma ambazo Qatar ilikanusha. Kuwait na Marekani zimekuwa wapatanishi katika mzozo huo.
