Ndayishimiye ataka mazungumzo na vyombo vya habari vilivyoadhibiwa yaanze


Rais Evariste Ndayishimiye ameahidi kumaliza migogoro iliyopita kati ya serikali na vyombo vya habariImage caption: Rais Evariste Ndayishimiye ameahidi kumaliza migogoro iliyopita kati ya serikali na vyombo vya habari

Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye ameitolea wito kamati ya udhibiti wa vyombo vya habari vinavyofanyia kazi nchini Burundi , CNC, kufanya mazungumzo na vyombo vya habari vilivyoadhibiwa ilikupata suluhu ya kudumu.

Vyombo vya habari vya kimataifa BBC na VOA vilipigwa marufuku kufanyia kazi nchini Burundi tangu mwezi Machi 2019 kwa tuhuma za kutangazi taarifa za uongo.

Akizungumza na wandishi wa habari nchini Burundi, Rais Evariste Ndayishimiye amesema kuwa ameazimia kumaliza mgogoro uliopo kati ya serikali na waandishi wa habari kipindi kilichopita.

Amesema: Ninachowaahidi ni kwamba ni mgogoro tuliokua nao siku zilizopita ambao tunapaswa kuupatia suluhu.

"Kuna vyombo vya habari vilivyochukuliwa hatua , naomba CNC kukaa pamoja mtafute suluhu, sote tuombe."

Rais Ndayishimiye amesema pia kwamba vyombo vya habari ni daraja lililo kati ya raia na uongozi kwasababu ndio wanaoonesha ni wapi mambo hayaendi vizuri ili uongozi ujirekebishe.

Mwishoni mwa mwezi wa Disemba 2020, Rais Ndayishimiye alisaini sheria inayotoa msamaha kwa waaandishi wa habari wanne wa radio Iwacu nchini humo, ambao walikuwa wamefungwa gerezani kwa siku 430.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi