Magaidi wadaiwa kumteka nyara na kumuua mkuu wa idara ya polisi mjini Aden

 


Mkuu wa Idara ya Polisi ya Mkoa wa Hudeyde Brigedia Jenerali Ibrahim Harid, ameripotiwa kuuawa mjini Aden nchini Yemen.

Akiongea na shirika rasmi la habari la SABA nchini Yemen, Rais Abdurabbu Mansur Hadi alitoa ujumbe wa rambirambi kwa Harid.

Akielezea kuwa Harid aliuawa shahidi katika shambulizi la kigaidi, Hadi alisisitiza kwamba magaidi waliofanya uhalifu huu hawawezi kuepuka adhabu.

Naibu Gavana wa Hudeyde Walid al-Kudeymi aliripoti kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba Harid alitekwa nyara mbele ya nyumba yake iliyoko Aden.

Taarifa za vyanzo vya habari vya ndani, zilisema kwamba mwili wa Harid uliokuwa na alama za mateso ulipatikana huko Aden.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi