Takukuru Manyara yaanzisha ofisi inayotembea


Na John Walter-Manyara

Ili kuwafikia wananchi katika kusambaza elimu ya mapambano dhidi ya rushwa na kupokea malalamiko, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Manyara imeanzisha ofisi inayotembea.

Utaratibu huo unaojulikana kama MOBILE PCCB unafanyika Mara moja kwa kila mwezi ambapo ofisi itawafuata wananchi walipo kwa lengo la kusikiliza pamoja na kutatua kero zao.

Mkuu wa Takukuru mkoani  Manyara Holle Makungu, amesema mpango huo umeanza kufanya kazi  kuanzia mwezi Januari 18,2021 katika kijiji cha Naisinyai mji mdogo wa Mirerani ambapo walisikiliza na kutatua kero katika kijiji hicho.

Mbali na hilo Takukuru inaendelea kuwakumbusha wananchi kutoa ushirikiano kwa kufichua vitendo au viashiria vya rushwa kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi yaani SMS kwa namba 113 au kupiga simu ya bure 113 au kufika katika ofisi za Takukuru zilizopo nchi nzima.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi