Serikali ya Zanzibar imetiliana Saini na Mamlaka ya Uwekezaji Oman kuhusu Mpango Mkuu wa Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani


 Na Thabit MADAI, Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imetiliana Saini na Mamlaka ya Uwekezaji Oman ya hati ya Maelewano (MOU), inayohusu Mpango Mkuu wa Ujenzi wa Bandari ya Mangapwani unaojumuisha Bandari tofauti ikiwemo bandari ya mizigo, uvuvi, mafuta na gesi asilia, chelezo pamoja na Mji wa kisasa ambapo Rais wa Znzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alishuhudia.

Akizungumza mara baada ya ujiaji wa saini hiyo, Rais Dk Mwinyi, alisema dhamira ya kuijenga Zanzibar inaendelea na kwa sasa serikali inaanza kujenga bandari ili kuendeleza uchumi wa Zanzibar.

Alisema bandari hiyo haitokuwa na Makontena pekee bali itakuwa bandari yenye terminal nyingi, ikiwemo eneo la mafuta, gesi, uvuvi na chelezo na kufanyia matengenezo ya meli.

Alisema,kuwa kazi iliyokuwepo sasa ni kuendelea na mipango iliyokuwepo katika mkataba huo ili kuweza kumalizika kwa wakati.

Akizungumzia bandari ya Mpiga Duri, Dk. Mwinyi, alisema kuwa ujenzi wa bandari hiyo upo pale pale na haijafutwa ila kwa sasa serikali itatengeneza bandari kubwa ya Uvuvi, ambapo siku zijazo kutafanyika makabaliano na wawekezaji wengine ili kuanza ujenzi wake rasmi ambao itahusisha miundombinu na viwanda

“Bandari na Mpiga Duri itauwa tofati kabisa kama tulivyosema hapo awali ambao mategemeo yangu tutaposaini kazi itaanza” alisema.

Sambamba na hao, alisema kuwa kwa sasa mpango ulikuwepo kuifanya bandari ya Malindi kuwa ni ya Utalii kwani eneo lake ni dogo na limo ndani ya sehemu ya mji Mkongwe uliohifadhiwa.

Akitoa maelezo kabla ya kusaini hati hiyo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Rahma Kassim Ali, alisema, ujenzi huo unatarajiwa kufanyika Mangapwani/Bumbwini ni moja ya dhana sahihi ya kuimarisha uwekezaji na hatimae kuleta matokeo bora kwa wananchi wa Zanzibar.

Alisema utiaji saini hati ya Maelewano inayohusu Mpango Mkuu wa Ujenzi katika Bandari ya hiyo ya Mangapwani ni miongoni mwa hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar awamu ya nane katika kutekeleza Sera yake ya Uchumi wa Buluu.

Alisema kuwa kamati ya mpango huo umezingatia, maelekezo ya serikali, sera na sharia mbalimbali za nchi kwa kuzingatia maslahi mapana ya Zanzibar kwa sasa na siku zijazo.

“Tumekubaliana mpango huu uwe tayari umeshaandaliwa ndani ya mienzi sita, hivyo matumaini ya serikali utakwenda kama ulivyokusudiwa” alisema.

Aidha alisema kuwa Serikali ya awamu ya nane imefungua fursa mbalimbali za uwekezaji ambao serikali imekuwa ikichukua hatua madhubuti katika kusimamia uwekezaji wenye maslahi mapana ya wannachi wa Znzibar.

Sambamba na hao, alifahamisha kuwa mpango huo utajumuisha bandari ya Makontena na Mizigo mchanganyiko (Multipurpose Port), Bandari ya mafuta na Gesi (Liguid Bulk Terminal), Bnadari ya Kuhudumia Mafuta na Gesi Asili (Offshore service) Center Base) na Bandari yenye Miundombinu ya Chelezo.

Pamoja na hao, alisema kuwa, hatua hiyo ni miongoni mwa mafanikio makubwa ya Serikali ya awamu ya Nane chini ya uongozi wa Dk. Hussein Mwinyi kuelekea siku mia tokea alipoapishwa kushika wadhifa wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Utiaji Saini huo uliofanyika kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman kwa kumshirikisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Amour Hamil Bakari na upande wa Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman anaetarajiwa kusaini ni Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Sheikh Mohammed Al-Tooq ambaye ataongoza ujumbe wa watu watatu.


 

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi