Na Timothy Itembe Mara.
JESHI la polisi Tarime/Rorya linawshikilia watu wa tatu kwa makosa ya kukutwa wakisafirisha shehena ya madwa ya kulevya aina ya bangi kinyume cha sheria.
Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa mkoa wa kipolisi/Tarime/Rorya ,ACP,Wilyamu Mkonda alisema kuwa wanawashikilia watu watatu wakiwa wanasafirisha magunia ya Bangi yamechanganya na magunia ya mahidi kinyume cha sheria na upelelezi ukikamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yanayowakabili.
Kamanda huyo aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni pamoja na Salumu Issa 26 mkazi wa Nzega ambaye ni mnyiramba na mwingine,Khalidi Yusuph 44 mkazi wa Mwanza ambaye ni msukuma na watatu ni Amosi Chacha 29 makzi wa mtaa wa mkuyuni kata ya Turwa ambaye ni mkurya akiwa anasindikiza.
“Tumefanikiwa kukamata Gari aina ya SCANIA lenye namba za usajili T-456 DQJ na Trailea lenye namba za usajili T-143 DEM na dereva wake Salumu,Issa na konda wake Khalid Yusuph likiwa limepakia mzigo wa mahindi mabichi uliochanganywa na madawa ya kulevya aina ya bangi ndani yake huku likisindikizwa na msindikizaji wake Amosi Chacha hiuku liisafirishwa kinyume cha sheria kutoka Tarime kwenda Daresalamu”alisema Mkonda.
Mkonda aliongeza kusema gari hilo lilipakiliwa mzigo huo kijiji cha Nyamwigura na kukamatiwa kijiji cha Gamasara barabara ya kwenda Mwanza kuelekea Daresalamu na watuhumiwa wote watatu wanaendelea kuhojiwa taratibu za kuwapata wengine zinaendelea ambapo watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu mashitaka yanayowakabili.
Pia kamanda huyo alitumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa Tarime/Rorya wale wenye mapenzi mema na nchi yao kuendelea kutoa ushirikiana kwa jeshi la polisi ili kuendelea kufichua uhalifu na wahalifu ili kukamatwa na kushugulikiwa kisheria.
Naye mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Tarime ambaye ni mkuu wa wilaya,Mtemi Msafiri alisema kuwa magunia hayo yalikuwa yanasafirishwa kinyume cha sheria na ambapo wasamaria wema alitoa taarifa kwa vyombo husika kuwa kuna magunia ya bangi yanasafirishwa kinyume cha sheria ambapo walifuatilia wakakuta ni kweli na watuhumiwa kukamatwa.
Msafiri aliongeza kuwa baada ya gari hilo kukamatwa na kufikishwa kituoni polisi kilichopo Bomani bhuku likipekuliwa polisi walikuta ndani yake kunamagunia 80 ya bangi yakiwa yamefunikwa na magunia ya mahindi mabichi 95 na kuwa kitendo hicho cha kusafirisha bangi nikinyume cha sheria.
Mkuu wa wilaya hiyo alibainiasha kuwa taratibu za kufikisha magunia hayo kwa mkemia mkuu wa serikali ili kupima na kubainisha kama kweli ndani yake kuna bangi kinafanyika.
Msafiri aliwaambia waandishi wa habari kuwa polisiwalifanikiwa kukamata gari hilo kutokana na kupewa taarifa na wasamaria wema ambapo walifanikiwa kulikamata hapo januari 27,01,2021 majira ya saa,i.30 asubuhi likiwa nasafiri kutoka Tarime kuelekea Daresalamu.
