Baraza la Seneti Marekani lajiandaa kusikiliza kesi dhidi ya Donald Trump

 


Baraza la seneti linaanza rasmi leo kusikiliza mchakato wa kesi dhidi ya rais wa zamani Donald Trump. Mchakato huo wa kihistoria ni wa pili wa kutaka rais huyo wa zamani ashtakiwe. 


Timu ya mawakili wa Trump imetaka kesi hiyo itupiliwe mbali wakisema ni tukio la kisiasa unaochochewa na waendesha mashtaka wa chama cha Democratic na wala Trump hapaswi kulaumiwa kwa vurugu zilizotokea katika majengo ya bunge. 


Waendesha mashtaka wademokrat wanadai kiongozi huyo wa zamani alichochea vurugu nchini Marekani kwa makusudi. Baraza la wawakilishi mwezi uliopita lilipitisha hukumu ya kumshtaki Trump kuhusiana na dhima yake katika vurugu za Januari 6 ambapo bunge la Marekani lilitekwa nyara na wafuasi wa rais huyo. 


Leo maseneta 100 watahusika kusikiliza kesi dhidi ya Trump kama majaji. Kesi hiyo itakayoanza jioni ya saa kumi na moja kwa saa za Ulaya ya kati itafanyika wakati bunge la nchi hiyo likiwa bado limefungwa na kuwekwa ulinzi mkali ikiwa ni mwezi mmoja baada ya vurugu zilizotokea.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi