Kundi la V4 lafungua mjadala kuadhimisho miaka 30 ya kundi hilo


Marais wa Poland Hungary na Jamhuri ya Czech na Slovakia wamekutana huko kaskazini mwa Poland leo kushiriki katika mjadala wa siku mbili wa kuadhimisha miaka 30 ya Jumuiya isiyo rasmi ya ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi ya nchi nne za Ulaya mashariki na Ulaya ya kati au kile kinachojulikana kama V4 au kundi la Visegrad. 


Mazungumzo ya viongozi hao yatajumuisha suala la mapambano dhidi ya janga la virusi vya Corona, usalama wa nishati, ulinzi wa mazingira pamoja na suala la uhusiano wa kimataifa na Ulaya na Marekani.


 Wiki ijayo waziri mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki ataongoza mkutano wa viongozi wa kundi hilo la V4 wa maadhimisho hayo ya miaka 30 ya kundi hilo utakaofanyika pamoja na rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel katika kasri la Wawel mjini Krakow, kusini mwa Poland.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi