Mahakama yaahirisha kusoma hukumu anayedaiwa kusafirisha dawa za kulevya

 


Mahakama ya hakimu mkazi Arusha leo Jumatano Februari 3, 2021 imeahirisha tena kutoa hukumu ya kesi ya kusafirisha dawa za kulevya inayomkabili mkazi wa jijini Arusha, Mkami Shirima.


Mkami pia anakabiliwa na kesi nyingine ya kumuua mfanyakazi wake wa ndani,  Salome Zakaria(18).


Katika kesi hiyo hakimu mkazi,  Gwantwa Mwankuga amesema  Shirima anatuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya  aina ya Mirungi yenye uzito wa kilo 2.95 kinyume cha Sheria.


Mtuhumiwa  huyo anadaiwa  kutenda kosa hilo Septemba 24, 2019 katika  eneo la Mianzini  mkoani Arusha akiwa na mwenzake, Emaliana Laizer wakitaka kusafirisha kilo 2.9 za mirungi.


Hakimu huyo ameahirisha kusoma hukumu hiyo kutokana na kutokamilika huku Shirima akirejeshwa rumande.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items